Duration 3:28:59

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA : IBADA YA EVENING GLORY : FRIDAY PRAYERS 08 / 10 / 2021

8 289 watched
0
125
Published 8 Oct 2021

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA : IBADA YA EVENING GLORY : FRIDAY PRAYERS 08 / 10 / 2021 KICHWA CHA SOMO : KIKOMBE HIKI ( Gethsemane ,Njiapanda ya Hatima Yako ) UJUMBE WA LEO : KIKOMBE CHANGU KIMEFURIKA Zaburi 23 : 4 - 6 Luka 22 : 20 Mathayo 26 : 36 - 54 Luka 22 : 39 - 43 Zaburi 23 : 4 - 6 4 Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya; Kwa maana Wewe upo pamoja nami, Gongo lako na fimbo yako vyanifariji. 5 Waandaa meza mbele yangu, Machoni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika. 6 Hakika wema na fadhili zitanifuata Siku zote za maisha yangu; Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. Luka 22 : 20 20 Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu. Mathayo 26 : 36 - 54 36 Kisha Yesu akaenda pamoja nao mpaka bustani iitwayo Gethsemane, akawaambia wanafunzi wake, Ketini hapa, hata niende kule nikaombe. 37 Akamchukua Petro na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kuhuzunika na kusononeka. 38 Ndipo akawaambia, Roho yangu ina huzuni nyingi kiasi cha kufa; kaeni hapa, mkeshe pamoja nami. 39 Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifulifuli, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe. 40 Akawajia wale wanafunzi, akawakuta wamelala, akamwambia Petro, Je! Hamkuweza kukesha pamoja nami hata saa moja? 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu. 42 Akaenda tena mara ya pili, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe. 43 Akaja tena, akawakuta wamelala; maana macho yao yamekuwa mazito. 44 Akawaacha tena, akaenda, akaomba mara ya tatu, akisema maneno yale yale. 45 Kisha akawajia wanafunzi wake, akawaambia, Laleni sasa, mpumzike tazama, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anatiwa katika mikono ya wenye dhambi. 46 Ondokeni, twende zetuni! Tazama, yule anayenisaliti amekaribia. 47 Basi alipokuwa katika kusema, tazama, Yuda, mmoja wa wale Thenashara akaja, na pamoja naye kundi kubwa wenye panga na marungu, wametoka kwa wakuu wa makuhani na wazee wa watu. 48 Na yule mwenye kumsaliti alikuwa amewapa ishara, akisema, Nitakayembusu, huyo ndiye; mkamateni. 49 Mara akamwendea Yesu, akasema, Salamu, Rabi, akambusu. 50 Yesu akamwambia, Rafiki, fanya ulilolijia. Wakaenda, wakanyosha mikono yao wakamkamata Yesu. 51 Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio. 52 Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. 53 Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? 54 Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri? Luka 22 : 39 - 43 39 Waandishi wengine wakajibu wakamwambia, Mwalimu, umesema vema; 40 wala hawakuthubutu kumwuliza neno baada ya hayo. 41 Akawaambia, Wasemaje watu kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi? 42 Maana, Daudi mwenyewe asema katika chuo cha Zaburi, Bwana alimwambia Bwana wangu, Uketi mkono wangu wa kuume, 43 Hata niwaweke adui zako Kuwa kiti cha kuwekea miguu yako. Mhubiri: Mwl. Gadielson Mfinanga Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

Category

Show more

Comments - 21
  • @
    @siakiwelu32553 years ago Ninajua tena kwa hakika mungu ataibadilisha taabu yangu.
  • @
    @emanuelmartin34173 years ago Ubalikiwe sana mtumishi kwa ibada nzuri. 1
  • @
    @lizaraul30673 years ago Huo ushuhuda umeniguza sana, mungu apewe sifa. Neema na fadhili zitanifuata milele, amen.
  • @
    @phoebemmanga60473 years ago Amen. Ee mwenyezi mungu naomba ugeuze matanga yangu kuwa machezo. Unuliwe zaidi mwl. Mfinanga wiki hii imekuwa ya faraja ktk madhabahu ya kikushi ikiongozwa na mch. Eliona kimaro.
  • @
    @emmanuelmsangi77933 years ago Old is gold!
    kijitonyama uinjilisti mmetukumbusha mbali!
    huduma yenu iwe ukumbusho mbinguni!
    kwaya ya uinjilisti kibangu tumewamiss! tutakutana tamasha la dayosisi, jimbo la kaskazini tumehamishwa!
    teh! Teh!
    j' pili tunawaiga hakyanani! Za zamani zilikuwa na wingu!
    mzee masaki ataimba " unishike mkono"
    .
    ...Expand
    1
  • @
    @gifthumphrey31233 years ago Mungu akubariki sana mwl mfinanga. Nimebarikiwa sana na ushuhuda wa dr rev kimaro na ibada nzima, though i am miles away i could still feel the presence . ...Expand