Duration 18:5

TAMASHA KUBWA LA NYAMA CHOMA KUFANYIKA MNADA WA MSALATO, DODOMA

134 watched
0
3
Published 8 Dec 2021

Na Richard Mwaikenda, Dodoma. TAMASHA la Nyama Choma linatarajiwa kufanyika katika Mnada maarufu wa Msalato, jijini Dodoma Jumamosi Desemba 11, 2021. Tamasha hilo linaloratibiwa na Diwani wa Kata ya Msalato, Nsubi Bukuku kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi wa kata hiyo, pamoja wachoma nyama wa eneo hilo, litaendeshwa kwa mtindo wa kuwashindanisha na watakaoshinda watazawadiwa yawadi kem kem. Ili kufanikisha tamasha hilo, Bodi ya Nyama Tanzania imeamua kuendesha mafunzo kwa wadau wa soko hilo jinsi ya kuandaa nyama kutoka machinjioni, kusafirisha, kuhifadhi na usafi wakati wa kuchoma na hatimaye kumuuzia mteja iliyo safi na salama. Mafunzo hayo zameendeshwa na Daktari wa Mifugo wa Bodi hiyo, Olais Ngilisho.

Category

Show more

Comments - 0