Duration 1:37:8

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA EVENING GLORY

3 639 watched
0
69
Published 8 Apr 2021

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA IBADA YA EVENING GLORY 08/4/2021 "UNAONA NINI?" "WHAT DO YOU SEE?" Yeremia 1 : 11 -12 Mwanzo 37 : 15 - 22 2 Wafalme 4 : 16 -17 Mathayo 14 : 26 - 33 Marko 4 : 35 - 41 Yeremia 1 : 11 -12 11 Tena neno la Bwana likanijia, kusema, Yeremia, waona nini? Nikasema, Naona ufito wa mlozi. 12 Ndipo Bwana akaniambia, Umeona vema, kwa maana ninaliangalia neno langu, ili nilitimize. Mwanzo 37 : 15 - 22 15 Mtu mmoja akamkuta, naye alikuwa anazunguka-zunguka katika nyika; yule mtu akamwuliza, akisema, Unatafuta nini? 16 Akasema, Nawatafuta ndugu zangu; tafadhali uniambie mahali wanakochunga. 17 Yule mtu akasema, Wametoka hapa, maana niliwasikia wakisema, Twendeni Dothani. Basi Yusufu akawafuata ndugu zake akawakuta huko Dothani. 18 Wakamwona toka mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue. 19 Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja. 20 Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika birika mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake. 21 Reubeni akasikia akamwokoa katika mikono yao, akasema, Tusimwue. 22 Reubeni akawaambia, Msimwage damu; mtupeni katika birika hii iliyopo nyikani, wala msimguse; ili apate kumwokoa katika mikono yao, akamrudishe kwa baba yake. 2 Wafalme 4 : 16 -17 16 Akasema, Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana. Akasema, La! Bwana wangu, wewe mtu wa Mungu, usiniambie mimi mjakazi wako uongo. 17 Yule mwanamke akachukua mimba, akazaa mtoto mume wakati uo huo mwakani, kama Elisha alivyomwambia. Mathayo 14 : 26 - 33 26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu. 27 Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope. 28 Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji. 29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu. 30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe. 31 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka? 32 Nao walipopanda chomboni, upepo ulikoma. 33 Nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu. Marko 4 : 35 - 41 35 Siku ile kulipokuwa jioni, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng'ambo. 36 Wakauacha mkutano, wakamchukua vile vile alivyo katika chombo. Na vyombo vingine vilikuwako pamoja naye. 37 Ikatokea dhoruba kuu ya upepo, mawimbi yakakipiga chombo hata kikaanza kujaa maji. 38 Naye mwenyewe alikuwapo katika shetri, amelala juu ya mto; wakamwamsha, wakamwambia, Mwalimu, si kitu kwako kuwa tunaangamia? 39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu. 40 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga? Hamna imani bado? 41 Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii? Mhubiri : Ev. Henry Mlay Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

Category

Show more

Comments - 2