Duration 1:57:33

KIKAO CHA WAKULIMA - SEHEMU YA PILI

883 watched
0
13
Published 18 Nov 2021

KATIKA KIKAO CHA WAKULIMA Kampuni ya JATU PLC tarehe 13.11.2021 ilifanya kikao cha wakulima katika ofisi za Jatu saccos zilizopo Dar es salaam, sabasaba maonesho. Mkutano huu ulihudhuriwa na viongozi wa Jatu plc wakiongozwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi, mkurugenzi mtendaji, viongozi wa Jatu Saccos Ltd, pamoja na wanachama wakulima wa Jatu plc. Katika mkutano huu ajenda nyingi zilijadiliwa na yafuatayo ni maazimio yaliyofikiwa. 1. Kuhusu zuio la asilimia 2 (withholding tax) kwa wakulima, tulikubaliana tuendelee kuzuia hiyo asilimia 2 hadi pale serikali itakapo toa tamko la mwisho tukizingatia kwamba kuna mswada umepelekwa bungeni kuhusu kubadili sheria hiyo ambayo inapendekeza kuondoa zuio hilo kwa wakulima. 2. Kuhusu maandalizi ya kilimo msimu wa mwaka 2021-2022, wakulima walishauriwa na kukubali kukamilisha taratibu za kushiriki kilimo kwa wakati ikiwa ni pamoja na kukodi mashamba na kuweka akiba kwa wakati ili kuwezesha utekelezaji kufanyika kwa wakati mashambani. 3. Kilimo cha zao la SOYA kwa ajili ya soko la CHINA kilijadiliwa na kupitishwa na wakulima wote na kwamba kuanzia tarehe 01.12.2021 kupitia app ya jatu market watu wataanza kuweka oda ya kukodi mashamba kwa ajili ya kilimo cha soya kitakacho fanyika mkoa wa rukwa sumbawanga na kwa sababu hii tulikubaliana maharage ya kawaida yaendelee kulimwa mkoa wa Tanga kilindi kwa ajili ya soko la ndani na maharage aina ya soya yalimwe sumbawanga kwa ajili ya soko la kimataifa. Pia tulikubaliana mwisho wa kukodi mashamba kwa ajili ya zao la maharage kilindi itakuwa tarehe 30.11.2021 ili kuruhusu sasa kampuni iweke nguvu kubwa kwenye zao la soya ambalo tayari limepata soko la uhakika kimataifa. 4. Kuhusu mradi wa chungwa unao endelea mkoa wa Tanga taarifa ilitolewa kwamba ukosefu wa mvua unaathiri ukuaji wa miche yetu na hivyo inahitajika juhudi ya ziada kukabiliana na changamoto ya ukame. Hili pia lilizungumzwa sambamba na maendeleo ya mradi wa parachichi ambao unaendelea vizuri katika mkoa wa njombe. Iliazimiwa kiandaliwe kikao maalumu kati ya uongozi wa jatu na wakulima wa mradi wa machungwa ili kujadili namna ya kutatua hiyo changamoto mapema iwezekanavyo. 5. Kuhusu ufugaji ufafanuzi ulitolewa kwa jinsi ambavyo mradi utaendeshwa na wakulima walikubaliana kuweka nguvu kubwa katika mradi huu kwani pamoja na faida nyingi zilizokuepo katika ufugaji pia ni mradi ambao utampa mapato makubwa na kwa muda mfupi mwanajatu, ilikadiriwa kwamba batch moja inaweza kuwa imekamilika kuanzia maandalizi hadi kuuza na mwanachama akapata pesa yake ndani ya miezi mitano tu ukilinganisha na kilimo. 6. Kuhusu bima ya mifugo na mazao wakulima na uongozi walikubaliana kwa pamoja kwamba kampuni ya bima ianzishwe na wao kama wadau muhimu wa kilimo wawe wana hisa wa mwanzo kwa utaratibu ambao utawekwa na kampuni ambapo ilikubaliwa kwamba kila mwanachama mwenye uwezo wa kuchangia shilingi milioni hamsini anaruhusiwa kuwa mwanahisa yeye binafsi au wanachama wasiozidi 30 wanaweza kuungana na kuanzisha kikundi chao aina ya kikoba kwa mfumo wa jatu ambacho kitaitwa JATU CLUB maalumu kwa lengo la kutumia jina la kikundi na wakajichanga wakapata mtaji wa milioni 50 au zaidi ili wawe wanahisa wa kampuni ya bima (JATU INSUARANCE CO. LTD) na uongozi wa jatu ulikubali na kuahidi kuandaa fomu maalumu kwa ajili ya wanachama wanaotaka kujiunga katika vikundi na kuchangia huo mtaji waanze kujaza kuanzia jumatatu hii, kila mwanachama anayehitaji kujiunga na kikundi sharti awe na uwezo wa kulipa shilingi million mbili kabla ya kusajiliwa katika kikundi hicho, lakini kwa wale wanachama wenye uwezo wa kulipa milioni 50 au zaidi wenyewe binafsi bila kuchangishana tayari fomu zimeandaliwa na katiba (MEMART) ya kampuni hiyo ya bima hivyo wanashauriwa kuwasiliana na idara ya sheria ya kampuni ili waweze kupewa utaratibu wa kujaza fomu hizo. Zoezi hili limeanza kutekelezwa na linategemewa kuwa limekamilika kufikia Desemba 2021. Wanahisa wanaohitajika katika kampuni hii ya bima ni wanahisa 50 tu ambao wanaweza kuwa aidha mtu binfasi au kikundi. (Natural or legal person). 7. Kuhusu masoko ya kimataifa uongozi ulitoa maelezo ya juhudi ambazo zinafanyika kuhakikisha tunaingia katika soko la kimataifa na ilikubaliwa kwa pamoja kwamba, mavuno ya msimu wa mwaka 2020-2021 hayatauzwa katika soko la kimataifa au kwa wazalishaji wengine wenye viwanda bali yatatumika kama mali ghafi katika soko la ndani kwa kupitia viwanda vya jatu plc. Lakini uongozi ulitoa muongozo kwa wakulima wote kwamba kuanzia msimu wa 2021-2022 mavuno yake yataandaliwa kwa ajili ya soko la ndani na la nje. 8. Kuhusu utaratibu wa kuuza mazao ya wakulima kwa msimu wa mwaka 2020-2021. ASANTENI SANA KWA KUTAZAMA. Please Subscribe, Share, Like, and Comment

Category

Show more

Comments - 3