Duration 16:4

Historia ya ALIKIBA, Alipozaliwa, Umri, Mapenzi na Maisha Yake

45 745 watched
0
405
Published 12 Jun 2018

Historia ya ALIKIBA, Alipozaliwa, Umri, Mapenzi na Maisha Yake Alikiba alizaliwa Iringa Novemba 26, 1986 kutoka kwa mama yake Tombwe Njere na baba yake Saleh Omari. Yeye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto wane katika familia yao, akifuatiwa na Abdu Saleh Kiba ambae ni mdogo wake huku wote wakifanya muziki wa bongo fleva. Muziki ni kati ya vitu ambavyo zimekuwa vikipendwa na mwanamuziki huyu tangu utoto wake. Asilimia kubwa ya wapenda burudani Afrika Mashariki kwa sasa wanazungumzia kuhusu ujio wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Salehe Kiba, maarufu kama Alikiba. Baadhi ya watu wamekuwa wakimlinganisha na mwanamuziki nyota kwa sasa Diamond Platnumz, ambaye naye kwa sasa yupo katika nafasi ya juu kimataifa kama ilivyokuwa kwa Alikiba miaka mitatu iliyopita. Si kwamba ndiyo anaingia katika muziki, kwa watu wanaojua historia ya bongo fleva wanakumbuka kwamba kijana alikuwa tishio, kwani amekuwapo kwenye gemu tangu mwaka 2004 na kufanikiwa kutoa wimbo wake wa kwanza ambao ulimtambulisha uliojulikana kama ‘Cinderella’. Baada ya kumaliza elimu ya kidato cha sita mwaka 2004, alianza kujituma katika muziki na kufanikiwa kuandika wimbo wake wa kwanza, ‘Maria’. Mwaka huohuo Alikiba alianza kutengeneza albamu yake ya kwanza. Ilipofika mwaka 2005, alipata ofa ya kwenda kuchezea soka la kulipwa nchini Uganda, lakini baadaye aliachana na mpira ili kuendeleza kipaji chake cha muziki. Mwaka 2007 alifanikiwa kuachia albamu iliyopewa jina la ‘Cinderela’, sambamba na kuachia wimbo huo redioni, ambao ulivuma na kusababisha albam hiyo kuuzika zaidi sokoni. Albamu hiyo ilikuwa ni kati ya albamu bora na iliyouza zaidi mwaka 2007 Afrika Mashariki. Tangu hapo akaanza kupokea mialiko mingi kutoka Kenya, Rwanda, Uganda na Burundi. Aliifanya Afrika Mashariki kumjua kwa muda mfupi kupitia vibao kadhaa vilivyokuwepo katika albamu hiyo kama MacMuga, Nakshi Mrembo, Njiwa na Mali Yangu. Install GlobalPublishersApp Android: http://bit.ly/2AAQe1d iOS: http://apple.co/2Assf4M Subscribe /c/uwazi FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis ... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari Visit https://globalpublishers.co.tz/, Subscribe /c/uwazi1 Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… /c/uwazi1 /c/uwazi1 /c/uwazi1 WEBSITE: https://globalpublishers.co.tz/ FACEBOOK: https://www.facebook.com/Globalpublis ... TWITTER: https://twitter.com/GlobalHabari INSTAGRAM: https://www.instagram.com/globalpubli ..

Category

Show more

Comments - 36