Duration 1:1:56

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA : IBADA YA MORNING GLORY 04 / 01 / 2022

5 707 watched
0
101
Published 4 Jan 2022

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA : IBADA YA MORNING GLORY 04 / 01 / 2022 KICHWA CHA SOMO: VITA LANGONI ( MWANZO WA MIEZI ) Wazo: "Endelea mbele, usikubali Kupunguziwa Mwendo" Waamuzi 5 : 8 Kutoka 12 : 1 - 2 Zaburi 105 : 4 Yeremia 17 : 5 - 8 Zaburi 11 : 3 Waebrania 11 : 10 Luka 8 : 25 Mithali 18 : 20 - 21 Zaburi 19 : 14 Wazo: Wazo: Endelea mbele, usikubali Kupunguziwa Mwendo Waamuzi 5 : 8 8 Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arobaini wa Israeli? Kutoka 12 : 1 - 2 1 Bwana akanena na Musa na Haruni katika nchi ya Misri, akawaambia, 2 Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu. Zaburi 105 : 4 4 Mtakeni Bwana na nguvu zake, Utafuteni uso wake sikuzote. Yeremia 17 : 5 - 8 5 Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana. 6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. 7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. 8 Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda. Zaburi 11 : 3 3 Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini? Waebrania 11 : 10 10 Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. Luka 8 : 25 25 Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii? Mithali 18 : 20 - 21 20 Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake. 21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. Zaburi 19 : 14 14 Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu. Mhubiri : Mwl. Eng. Goodluck Mushi Kwa maoni na ushauri Smu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

Category

Show more

Comments - 22